I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, November 1, 2010

WAGOMBEA UWAKILISHI NA UBUNGE KUTOKA CUF WAMESHINDA MAJIMBO YA PEMBA

Wagombea wa nafasi za uwakilishi na ubunge Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF wanaendelea kushinda katika majimbo mbali mbali kisiwani Pemba.

Matokeo ya hivi karibuni mgombea uwakilishi jimbo la Tumbe kwa tiketi ya CUF Rufai Said Rufai ameshinda jimbo hilo kwa kupata kura elfu tano 312 na kumshinda mpinzani wake wa karibu wa CCM Amour Khamis Mbarouk aliepata kura 470.

Matokeo ya ubunge jimbo la Mkoani Ali Khamis Seif wa CUF ameshinda jimbo hilo, jimbo la Mkanyageni Mohamed Habib Mnyaa wa CUF ameshinda jimbo la Mtambile mgomea wa CUF Masoud Abdala Salum ameshina ubunge jimbo hilo.

Jimbo la Kiwani mgombea ubunge wa CUF Abdala Haji Ali meshanda wa jimbo hilo, jimbo la Chambani mbunge ni Salum Hemed Khamis wa CUF. Mwandishi wetu Haji Nassoro kutoka Pemba

Na huko jimbo la Wawi mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CUF Hamad Rashid Mohame ameshinda kwa kupata kura elfu tano 321 na kumshinda mpinzani wake karibu kutoka CCM Daud Khamis Juma aliepata kura elfu mbili 255

1 comment:

  1. Decrease your protein intake, choose fattier cuts of meats and supplement your fat
    with coconut oil. Almost all of our liveblogs and livestreams, along with protein, at each meal.
    Paleo Diet recipes are simple to follow and make a real difference to your health.


    Here is my blog: paleo diet review

    ReplyDelete