I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, October 31, 2010

TUME YA UCHAGUZI TANZANIA IMEAHIRISHA UCHAGUZI WA MAJIMBO MANNE YA ZANZIBAR

Tume ya taifa ya uchaguzi NEC katika wilaya ya magharibi imeahirisha uchaguzi wa wabunge katika majimbo matatu ya wilaya ya magharibi kwa muda usiojulikana.

Akizungumza na Zenji Fm radio msimamizi wa uchaguzi NEC wilaya ya magharib Amina Talib Ali ameyataja majimbo hayo ni Magogoni, Mtoni na Mwanakwerekwe.

Amesema kuahirishwa kwa uchaguzi huo kunatokana na upungufu wa karatasi za kupigia kura zilizopokelewa kwa wagombea hao na kutaja upungufu huo ni wa kibinadamu…

Hata hivyo Amina amewataka wapiga kura katika majimbo hayo kutovunjika moyo na kuwataka kuzitunza shahada za kupigia kura hadi pale itakapotangazwa tarehe nyingine ya kufanyika uchaguzi huo.

Wakati huo huo tume ya uchaguzi ya taifa NEC imeahirisha uchaguzi katika jimbo la Wete kutokana na jina la mgombea ubunge wa chama cha TLP kutoonekana katika karatasi ya kupigia kura.

Hata hivyo kazi za upigaji kura katika mkoa wa Kaskazini Pemba zimendelea vizuri licha ya kujitokeza matatizo katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.

Katika jimbo la Ole kumejitokeza upungufu wa karatasi za kupigia kura kwa wabunge na rais wa jamhuri ya muungano Tanzania hali iliyosababisha kuchelewa kuanza kwa upigaji kura.

No comments:

Post a Comment