I made this widget at MyFlashFetish.com.

Sunday, September 26, 2010

MUASISI WA MAPINDUZI ZANZIBAR SAID ABDALLA NATEPE AMEFARIKI DUNIA

Mmoja wa viongozi 14 wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,Meja Jenerali Abdallah Said Natepe amefariki dunia jana mchana katika hospitali yajeshi Lugalo mjini Dar es Salaam.

Marehemu Natepe ni miongoni mwa viongozi wa mapinduzi kumbi na mbili waliofariki dunia ambao walifanikisha kufanikiwa kwa mapinduzi ya Januari 12, 1964 yaliyoindoa serikali ya kisultani visiwa vya Zanzibar,

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, kifo hicho kimetokea jana mchana kwenye hospitali hiyo kuu ya Jeshi la Wananchi.
Taarifa hiyo inamnukuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akieleza kushtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha mwanamapinduzi huyo na kumtumia salamu za rambirambi katibu mkuu wa CCM akielezea jinsi alivyoguswa na kifo hicho cha Mzee Natepe.

“Kifo kimemchukua mwanamapinduzi, mzalendo na mwanachama wetu mwaminifu katika kipindi ambacho taifa na chama bado kinamhitaji sana. Kifo kimetunyang’anya tunu wakati huu tunaoelekea uchaguzi mkuu; ni huzuni kubwa kwetu; ni majonzi makubwa na hatuna neno kubwa linaloweza kuelezea huzuni hii,” Rais Kikwete anakaririwa kwenye taarifa hiyo.

Rais alipokea taarifa za kifo cha Mzee Natepe jana mchana akiwa Njombe mkoani Iringa ambako yuko kwa ajili ya shughuli za kampeni.

Rais Kikwete pia ametuma salaamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu Natepe.

“Mzee Natepe amekuwa sehemu ya maisha yangu ya kisiasa, kijamii na amenipa malezi na maelekezo mengi nikiwa kama kijana wake na amekuwa moja ya nguzo yangu kubwa katika shughuli zangu za kisiasa na kikazi katika maeneo yote niliyotumikia nchi yangu,” alisema rais na kuelezea kwa masikitiko huzuni aliyonayo na kuwahakikishia kuwa yuko nao katika kipindi hiki kigumu.

“Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi ya kuishi na Mzee Natepe na kufanya naye kazi. Tunamuomba Mungu amlaze mzee wetu mahali pema peponi na kumpa pumziko la milele, amina”

No comments:

Post a Comment