I made this widget at MyFlashFetish.com.

Friday, September 3, 2010

BENKI YA WATU WA ZANZIBAR KUIMARISHA HUDUMA ZAKE

Benki ya watu wa Zanzibar PBZ, inakusudia kuweka mitandao itayowawezesha wateja wake wa ndani na nje ya nchi kupata huduma za kuweka, kutoa na kupokea fedha popote walipo.

Kaimu mkurugenzi wa PBZ Bw. Ame Haji Makame amesema hayo katika hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo huko hoteli ya Zanzibar Beach Rasort nje kidogo ya Zanzibar na kuhudhuriwa na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume na wateja wengine wa PBZ.

Amesema uwekezaji huo unahusisha uwekaji wa mashine za ATM, mtandao utakaowaruhusu wateja kutoa na kuchukua fedha katika matawi yote ya PBZ na mtandao wa kimataifa wa kutuma na kupokea fedha kwa njia ya haraka kutoka nje ya Tanzania.

Amesema PBZ pia inaendelea na ujenzi wa tawi la benki kwa ajili ya wateja wakubwa katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar ambalo linatarajiwa kumalizika baada ya miezi mitatu na ujenzi wa tawi jingine mjini Dar es Salaam unaotarajiwa kumalizika mwezi Novemba.

Aidha Bw. Haji ameitaja miradi mingine itakayoiwezesha PBZ kumudu soko la ushindani ni ujenzi wa tawi la Chakechake Pemba pamoja na kujiunga na mfumo wa kutuma na kupokea fedha wa Western Union.

Amesema mfumo huo utasaidia serikali katika upokeaji wa fedha kati ya Zanzibar na nchi nyingine duniani na unatarajiwa kumalizika baada ya miezi miwili

No comments:

Post a Comment