I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, April 29, 2010

AMETUMIA SHOKA KWA KUWAUWA WATOTO WAKE WATATU

Mwanamke mmoja katika mkoa wa Kilimanjaro ametumia shoka kwa kuwauwa watoto wake watatu na mmoja kumjeruhi usiku wa kumkia jana.

Tukio hilo limeibua simanzi miongoni mwa wakaazi wa eneo hilo ambao wamedai mwanamke huyo ni mgonjwa wa akili amekuwa na mvutano na mumewe mara kwa mara na anashikiliwa na jeshi la polisi.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya majirani wa familia hiyo wamesema kitendo hicho ni ukatili na mwanamke huyo alikuwa akinywa pombe na wakati mwengine alikuwa akichanganyikiwa na kuzungumza mambo yasioeleweka.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro Lukas Ngoboko amesema miongoni mwa watoto waliouwawa katika tukio hilo ni mlemavu wa viungo asiekuwa na akili na mtoto aliejeruhiwa amelazwa hospitali akiwa na hali mbay

MVUA ZA MASIKA ZALETA MAFURIKO DAR MTU MMOJA AFARIKI DUNIA


Madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali nchini ikiwemo mjini Dar es Salaam yameendelea kuwakumba wakaazi wa mji huo ambapo baadhi ya miundo mbinu imesombwa na maji huku baadhi ya watu hawajulikani walipo.

Mvua hizo zimekuwa zikinyesha kwa siku tatu mfululizo zimesababiosha kifo cha mtu mmoja mkaazi wa Temeke na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara kutokana na baaadhi ya barabara kujaa maji na kusababisha msongomano wa gari.

Aidha mvua hizo zimesababisha kusombwa baadhi ya madaraja.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania Dr. Arnest Kijazi amesema mvua hizo zinazoendelea kunyesha katika ukanda wa pwani ya Tanzania zitaendelea hadi mwisho mwa mwezi huu.

Dr. Kijazi amewataka wakaazi wa maeneo hayo kuchukua hatua za tahadhari

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume kesho anatarajiwa kushuhudia utiaji saini wa utengenezaji wa waya mpya wa umeme wa chini ya bahari wa megawati 100 kutoka Tanzania bara hadi Zanzibar.
Mkataba wa utekelezaji wa mradi huo utatiwa saini ikulu mjini hapa kati ya kampuni ya VISCAS ya Japan iliyoshinda tenda ya utengenezaji na uwekaji wa waya huo na afisi ya Changamoto za Milenia Tanzania inayofadhili mradi huo

Taarifa iliyotolewa na afisi ya Chamoto za Milenia kwa vyombo vya habari imesema balozi wa Marekani nchini Tanzania pia atahudhuria utiaji wa saini huo na viongozi wengine wa serikali ya mapinduzi Zanzibar na taasi ya Changamoto.
Kukamilika kwa mradi huo unaotarajiwa kugharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 28 kutakiwezesha kisiwa cha Unguja kupata umeme wa uhakika ambao utachangia shughuli za uwekezaj

BANK YA BODEA YAZIDI KUTOA MSAADA KWA ZANZIBAR


Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika BADEA na Mfuko wa Saudi Arabia zimeahidi kuendelea kuisaidia Zanzibar katika ujenzi wa miundombinu ya barabara na mategenezo ya uwanja wa ndege wa Pemba.
Uongozi wa taasisi hizo za kifedha umetoa ahadi hizo ulipokuwa na mazungumzo na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume, Ikulu mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo uongozi huo ulieleza kuwa tayari barabara zote tatu za Pemba zikiwemo barabara ya Wete-Gando, Wete-Konde na Chake -Wete ambazo wanazigharami zimo katika mpango wa ujenzi.
Aidha, taasisi hizo pia zimeelezea nia yao ya kugharamia ujenzi wa barabara za Mwera-Pogwe-Jumbi, Cheju-Unguja Ukuu na Miwani-Kizimbani.
Nae rais Karume amesem serikali katika kuimarisha sekta ya mawasiliano ikiwemo miundombinu ya barabara pia, imeweka mikakati ya kuimarisha sekta ya kilimo hasa cha umwagiliaji maji.

Benki ya BADEA inaendelea kusaidia ujenzi wa majengo mapya ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA huko Tunguu wilaya ya Kati ambapo kukamilka kwa ujenzi huo kutasaidia kuimarisha sekta ya elimu nchini

MUANDISHI ZNZ ATUMIWA SMS ZA VITISHO


Mwaandishi mwandamizi anaefanyia kazi katika kampuni ya IPP media Maulid Hamad Maulid ameelezea kutumiwa ujumbe mfupi wa vitisho katika simu yake ya mkononi unaohatarishan maisha.
Akizungumza na waandishi wa habari huko idara ya habari Zanzibar amesema ujumbe huo ametumiwa baada ya kutoa taarifa zinazohusiana na migogoro ya ardhi ambayo inatokea katika kisiwa cha Unguja ambayo inaathiri kundi kubwa la wananchi.
Amesema kutokana na hali hiyo tayari amesehatoa taarifa kwa jeshi la polisi na mkurugenzi wa upelelezi na kuahidi suala mwa mwandishi huyo watalifanyia kazi.
Maulid Hamadi amekuwa akitoa taarifa ya Migogoro ya ardhi katika maeneo mbali mbali ikiwemo, Muyuni C, Kijiji cha Pwani mchangani, msitu wa hifadhi Kibuteni, Bumbwini Kiongwe pamoja na Fuoni Kibondeni.

Wednesday, April 28, 2010

KITENGO CHA KICHOCHO,MATENDE NA MINYOOO ZANZIBAR KIMESEMA UGONJWA WA MATENDE ZANZIBAR UMEWEZA KUPUNGUA CHINI YA ASILIMIA MOJA


Kitengo cha kichocho,matende na minyooo Zanzibar kimesema ugonjwa wa matende Zanzibar umeweza kupungua chini ya asilimia moja ya vimelea katika miili ya wagonjwa wanaougua hapa Zanzibar.
Akizungumza na zenji fm radio Meneja wa kitengo hicho Dr.Khalfan Abdallah Mohammed amesema mafanikio hayo yamekuja kutokana na jitihada kubwa walizozichukua ikiwa pamoja na ugawaji wa dawa kila mwaka katika wilaya mbali mbali za Zanzibar.
Amesema mbali ya ugawaji wa dawa elimu mbali mbali zimekuwa zikitolewa kwa wananchi juu kufahamu dalili za ugonjwa huo na kufika vituo vya afya kwa kupata matibabu muafaka.
Ameyataja maeneo yayoathirika zaidi na ugonjwa huo kuwa ni Mkoa wa kusini Unguja na Mkoa wa kusini Pemba…).
Amesema kutokana na mafanikio hayo kitengo hicho hivi sasa wataendeleza uchunguzi kwa kila mwaka kuangalia hali inaendeleaje sambamba na kuwashughulikia wale ambao wameathirika na ugonjwa huo.
Aidha ameitaka jamii kuondokana na imani potofu kwamba ugonjwa huo ni waurithi na baadala yake ugonjwa amesema ugonjwa huo unatonakana na kuenezwa na mbuu

WAISLAM ZANZIBAR KUANDAMANA


Jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu Zanzibar inatarajia kufanya Maandamano makubwa yenye lengo la kupinga uvunjaji wa minara ya miskiti nchini Uswiss .
Akizungumza na zenji Fm radio katibu wa jumuiya hiyo Sheikh Abdalla Saidi amesema maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 30.04.2010 ambayo yataanzia Masjid Mbuyuni baada ya sala ya Ijumaa kupitia kinazini na kuishia viwanja vya Lumumba.
Amesema maandamano hayo ni muhimu kwa vile huu ni wakati ambao waislamu wanatakiwa kuonyesha umoja wao kwa kupinga udhalilishaji dhidi ya dini yao……
Sheik Abdallah ametoa Wito kwa waislamu kushiriki kikamilifu katika pinga suala hilo ambalo limekuwa likidhalilisha uislamu kwa miaka mingi.

ZSSF WAJIBU CHAMA CHA WAFANYAKAZI ZNZ

Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF umesema sababu zilizochangia kuchelewa kutoa mafao ya uzazi na mafao ya matibabu ni kutokana na mfuko huo kuwa na uhaba wa raslimali zake .
Akizungumza na zenji Fm Radio afisa uhusiano wa mfuko huo Mussa Yussuf amesema uamuzi huo umetolewa baada ya wataalamu kutoka shirika la kazi ulimwenguni ILO Kufanya tathmini ya uwezo wa mfuko huo na wameishauri serikali kusitisha utoaji wa mafao hayo ili kuunusuru mfuko huo kufilisika.
Amesema kutokana na hali hiyo waziri anaehusika na fedha na uchumi ambae kwa mujibu wa sheria ya mfuko huo anauwezo wa kusitisha kutoa mafao hayo…
Afisa huyo ametoa ufafanuzi huo kutokana na madai yaliyotolewa na katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Zanzibar Zatuc Khamis Mwinyi akidai kusikitishwa na uchelewaji wa kutolewa kwa mafao ya uzazi na matibabu na mfuko huo.

ZANZIBAR


Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar imesema maradhi yasiyo ya kuambukiza yamezidi kuongeza hapa nchini kutokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha hapa Zanzibar.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Tiba na mratibu wa maradhi yasiyoambukiza wa wizara ya Afya na ustawi wa jamii Zanzibar Dr.Abdalla Juma Mabodi akizungumza katika warsha yakujadili namna ya kujinga na kuzuiya maradhi hayo iliyofanyika Manson Hotel mjini Zanzibar .
Dr.Mabodi amesema maradhi yasiyokuwa ya kuambukiza kama sindikizo la damu Kansa, Kisukari, Kiharusi, maradhi ambayo yameibuka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo huleta athari katika mwili na kusababisha maradhi hayo……
Aidha amesema maradhi ya kuambukiza kwa hapa Zanzibar yamepungua kwa kiasi kikubwa na kujitokeza kwa kasi maradhi yasiyoambukiza ambayo huleta maafa na vifo.
Mkutano huo umeshirikisha wajumbe kutoka nchi mbali mbali za Afrika ikiwa Zanzibar ni mwenyeji wa mkutano huo.

18 WAFARIKI DUNIA HAPO HAPO AJALI YA GARI (TANGA)


Watu 18 wamefariki dunia papo hapo na wengine 125 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la Mabanda ya Papa mjini Tanga.
Basi hilo lilikuwa limebeba wanafunzi wa chuo cha kiislamu Shamsu Maarifa waliokuwa wakisafiri kwa Lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T.757 BDB.
Kwa mujibu wa Daktari mkuu wa hospitali ya Bomba Mkoani Tanga amesema majeruhi watatu kati ya 125 hali zao ni mbaya na wanafanyiwa taratibu ya kupelekwa katika hospitali ya Mifupa ya Moi Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Nae kaimu kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani humo Adofsina Kapusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza taarifa zimesema kwamba chanzo cha ajali hiyo inatokana na mwendo wa kasi…
Hadi sasa maiti tisa zimeshatambuliwa na jamaa zao ambapo mazishi ya maiti hizo yamefanyika katika chuo hicho cha Shamsu Maarifa

Tuesday, April 27, 2010

MAREKANI KUISAIDA ZANZIBAR KATIKA MRADI WA WAYA MPYA WA UMEME WA MEGAWATI 100


Marekani imesema itaendelea kuunga mkono mpango wa nishati wa Zanzibar kwa kusaidia mradi wa waya mpya wa umeme wa Megawati 100 kupitia shirika la nchi hiyo la changamoto la Mellenium.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenna amesema mkataba wa mradi huo wa kuweka waya wa kupitishia umeme kutoka Tanzania bara unatarajiwa kutiwa saini mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza na rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa bartaza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume balozi Lenna amesema mradi huo ni mkubwa kuwahi kufadhiliwa na shirika la Changamoto la Marekani.
Amesema waya huo wa aina yake utatengenezwa nchini Japan na utumika kwa muda mrefu yakiwemo matumizi ya mawasiliano ya Internet ambayo yatasaidia kuchangia maendeleo ya uchumi wa Zanzibar.
Nae rais Karume emeishukuru serikali ya Marekeni kupitia shirika la Changamoto kwa ufadhi wa mradi huo ambao utasaidia maendeleo ya kiuchumi Zanzibar.
Hivi karibuni waziri wa maji, ujenzi, nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid amesema kisiwa cha Unguja bado kinakabiliwa na tatizo la umeme licha ya matengenezo makubwa yalifanywa kwenye waya wa sasa unaoleta umeme kutoka Tanzania bara.
Amesema waya huo wa megawati 45 licha ya kumalizika kwa muda wake, umezidiwa na matumizi na kuwataka wananchi kujiepusha na matumizi yasiokuwa ya lazima.

SAKATA LA ZATUC

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Zanzibar ZATUC linakusudia kuwashawishi wanachama wao kutochangia mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF kutokana na mfuko huo kutotimiza ahadi katika utoaji wa mafao ya uzazi na ugonjwa kwa wananchama wake.
Akizungumza na zenji fm radio katibu mkuu wa ZATUC Khamis Mwinyi Mohammed amesema mfuko huo kwa muda mrefu sasa umeshindwa kutoa mafao hayo huku ukiendelea kuwachanganisha wanachama wake.
Amesema kwa vile shirikisho lao lina mjumbe katika bodi ya ZSSF wanafikiria kumtoa mjumbe huyo ili kuepuka kushirikishwa katika mpango huo wa ZSSF unaokwenda kinyume na sheria za kuanzishwa kwa mfuko huo kwa kukosa kulipa mafao hayo
Mfuko wa ZSSF ulioanzishwa mwaka 1998 hivi unaendelea kutoa mafao ya uzeeni kwa wananchama wake wanaostaafu kazi.

CUF NA CHADEMA VIMONEKANA NDIO VYAMA PEKEE VYENYE KULETA UPINZANI NCHINI.


Matokeo ya utafiti yaliofanywa na mpango wa elimu wa chuo kikuu cha Dar es salaam REDT juu ya maoni ya wananchi katika uchaguzi mkuu ujao yameonesha iwapo uchaguzi huo ungefanyika sasa chama cha Mapinduzi CCM kingeibuka na ushindi katika urais, ubunge na madiwani.
Taarifa ya utatifi huo uliofanyika mwezi uliopita uliotolewa leo mjini Dar es Salaam kwa wandishi wa habari na mtafiti mkuu wa REDT Dr. Benerdeta.
Amesema asilimia 60 ya wa bunge wa sasa wa majimbo wangalipoteza viti vyao kwa kutowajibika ipasanyo katika majimbo yao
Aidha Dr. Benerdeta amesema vyama vya
Utafiti huo ulizihusihsa wilaya 52 nchini, huku asilimia 60 ya wananchi waliohojiwa ni wakaazi wa vijini na asilimia 40 ni wale mjini.

Monday, April 26, 2010

MATATIZO YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR YANATOA CHANGAMOTO YA KUIMARISHA MUUNGANO HUO ZAIDI.


Waziri wa mawasiliano na uchukuzi Zanzibar Brigedia mstaafu Adam Mwakanjuki amesema matatizo ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanatoa changamoto ya kuimarisha muungano huo zaidi.
Akizungumza na Zenji fm radio juu ya mafanikio ya miaka 46 ya muungano amesema matatizo hayo yanaweza kuondoshwa na watanzania wenyewe hatua kwa hatua baada ya kulaumiana kwa kila upande.
Amesema muungano wa Tanzania ni wakupigiwa mfano katika nchi nyingi duniani zilizoungana ambapo hivi sasa muungano huo haupo tena, hivyo ni vyema kwa watanzania kuendelea kuudumisha muungano wao...Bonyeza hapa kumsikia Brigedia mstaafu Adam Mwakanjuki
Aidha waziri Mwakanjuki amesema haja ya kuwepo muungano ipo na kuwataka wale wanaokosoa kupelekea agenda zao katika kamati maalum baada ya kuendelea kulalamika.
Waziri Mwakanjuki ambae hajaonekana hadharani kwa miezi kadhaa yuko katika likizo ya ugonjwa baada ya kupata ajali mkoani Dodoma akiwa katika majukumu ya kutekeleza shughuli za chama tawala cha CCM.

RAIS WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE AMETOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA ELFU TATU 101 KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 46 YA MUUNGANO.


Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa elfu tatu 101 katika kuadhimisha miaka 46 ya muungano.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kutiwa saini na waziri wa mambo ya ndani Laurent Masha imesema msamaha huo unawahusu wafungwa wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano, wenye magonjwa kama vile ukimwi, kifua kikuu na saratani.
Msamaha huo pia utawahusu wafungwa wazee kuanzia miaka 70, wafungwa wa wakike waliofungwa wakiwa wajawazito, walioingia kifungoni wakiwa na watoto wachanga na wenye ulemavu wa mwili na akili.
Aidha mshamaha huo wa rais hautawahusu wafungwa waliohukumiwa kunyongwa na adhabu hiyo itabadilishwa kuwa kifungo na wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha.
Wafungwa wengine ni wale wanaotumikia kifungo cha dawa za kulevya, rushwa, kunyanganya na kutumia silaha pamoja na wafungwa wanaotumikia kifungo cha kupatikana na silaha.
Wafungwa wengine amabao hauhusiki na msamaha huo wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujamiana, waliowapa ujauzito wanafunzi wa skuli za misingi, wizi wa miundo mbinu na wale waliotoroka chini ya ulinzi.

Wakati huo huo Viongozi wa dini nchini wamewaombea dua watanzania kujiepusha na siasa za kidini, ukabila, chuki na ueneo ili uchaguzi wa mwaka huu ufanyike kwa amani, haki na uhuru.
Wakiomba dua katika sherehe za maadhimisho ya miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dar es Salaam wamesema siasa za aina hiyo zinaweza kuvuruga amani na umoja wa Tanzania.
Kiongozi kutoka dini ya Kislamu Alhaji Mussa Salum amesema watanzania wanaendelea kufaidika na matunda ya muungano na kumuomba mwenyezi Mungu uchaguzi mkuu ujao ufanyike kwa amani na utulivu …
Nae askofu Sastari Lebena na Steven Manana wamesema wakati huu Tanzania inapoadhimisha miaka 46 ya muungano na kuelekea katika kipindi cha uchaguzi mkuu amewaombea watanzania kuwa na uvumilivi ili kuchagua viongozi wenye uchungu na nchi yao…
Uongozi wa Zenji fm radio na wafanyakazi wake inawatakia kila la kheir watanzania wote katika kuadhimisha miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

WATANZANIA LEO WAMEADHIMISHA SHEREHE ZA MIAKA 46 TANGU KUUNDWA MUUGANO WA NCHI MBILI ZA TANGANYIKA NA ZANZIBAR


Watanzania leo wameadhimisha sherehe za miaka 46 tangu kuundwa Muugano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Rais wa Tanzania na amiri jeshi mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama Jakaya Mrisho Kikwete katika maadhimisho hayo amepokea na kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi hivyo na kupigwa mizinga 21.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na maelfu ya watanzania na viongozi wengine serikali na vyama vya siasa akiwemo rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na mabalozi wa nchi za nje waliopo Tanzania.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa na rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume na rais wa Tanganyika Mwalim Julius Kambarage Nyerere.
Miongoni mwa mambo muhimu yaliosababisha viongozi hao kuunganisha nchi zao ni kutaka kuleta umoja wa bara zima la Afrika....

ULIPAJI WA KODI BADO NI TATIZO ZANZIBAR


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema bado tatizo la wafanya baishara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbili wanaposafirisha bidhaa zao Tanzania bara halijapatiwa ufumbuzi kutokana udhaifu wa watendaji.
Akizungumza na Zenji Fm radio juu ya mafanikio ya miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanizbar waziri wa nchi afisi ya waziri kiongozi Hamza Hassan Juma amesema serikali inasikitishwa na tatizo hilo kwa vile imekuwa ikitoa maagizo, lakini utekelezaji wake ni mdogo.
Amesema anashangazwa na mizigo inayopiliwa ushuru Tanzania bara na inapukuja Zanzibar hailipiwi ushuru tena, lakini hali hiyo inakuwa tofauti na mizigo ya biashara inayokwenda Tanzania bara ambayo pia hukwama kwa siku kadhaa…Bonyeza hapa kumsikia Bwana -HAMZA
Waziri Hamza amesema serikali inafahamu TRA ni moja ya taasisi inayokusanya mapato ya Zanzibar yanayoingia katika mfuko mkuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, lakini upande wa Tanzania bara taasisi hiyo haiwetendei haki wafanyabiashara wa Zanzibar.

Hata hivyo amesema katika kikao kilichomalizika hivi karibuni serikali ilitoa agizo kwa maafisa wa Zanzibar kukaa pamoja na maafisa wa TRA Tanzania bara ili kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.
Aidha waziri Juma amesema suala hilo pia linatarajiwa kuzungumzwa katika kikao cha mawaziri wa Zanzibar na Tanzania kitakachofanyika tarehe tatu mwezi ujao na baade kuitishwa kikao cha kero za muungano…..CLIPS…… KODI
Tatizo la wafanyabiashara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbili wakati wanapopeleka bidhaa zao Tanzania bara limekuwa la muda mrefu na kuleta usumbufu kwa wafanyabiashara hao.

Saturday, April 24, 2010

VYAMA VIDOGO VYA SIASA ZANZIBAR VYATISHIA KUJITOA KWENYE UCHAGUZI 2010

Chama cha siasa cha NLD kimeanza kuvishawishi vyama vingine vidogo vya siasa kususia uchaguzi mkuu wa Zanzibar kutokana na tume ya uchaguzi kutangaza viwango vikubwa vya fedha za dhamana kwa wagombea wa vyama watakaoshiriki katika uchaguzi huo.

Akizungumza na Zenji Fm Radio juu ya taarifa hiyo ya tume iliyotolewa kwenye vyombo vya habari naibu katibu mkuu wa NLD Zanzibar Rashid Ahmmed amesema uwamuzi huo utawafanya matajiri kutumia fedha zao kushiriki kugombea nafasi za uongozi na kuwacha wale wasiokuwa na uwezo wa kifedha.

Amesema chama cha NLD kinapinga viwango vya fedha za dhamana vilivyotangazwa na tume kwa vile havitoi fursa kwa wagombea wa vyama vidogo ambavyo havina ruzuku kushiriki katika uchaguzi huo wa demokrasia.

Bw. Ahmmed amesema tangazo hilo la tume ya uchaguzi litalipa nafasi zaidi vyama vinavyopewa ruzuku na serikali ambavyo ni CCM, CUF na CHADEMA na kusema hatua hiyo sio demokrasi ya vyama vingi…

Aidha naibu katibu mkuu huyo wa NLD amesema pamoja na tume ya uchaguzi haiwezi kushtakiwa kisheria, lakini wananchi wenyewe ndio watakaofanya maamuzi juu ya taarifa ya tume hiyo ya kuongeza viwango vya dhamana kwa wagombea wa urais, uwakilishi na udiwani.

Jana tume ya uchaguzi Zanzibar iltoa taarifa ya kupandisha dhamana kwa wagombea wa kiti cha urais wa Zanzibar kutoka shilingi milioni moja hadi milioni tatu, nafasi ya uwakilishi kutoka elfu 50 hadi laki tatu na udiwani kutoka elfu 15 elfu 50.

Akizungumza na Zenji Fm radio afisa habari wa tume hiyo Idriss Haji Jecha amesema kiwango hicho kimeongezwa kutokana na hali ya kifedha ya watu wanaotaka kugombania urais na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.

Uchaguzi mkuu wa Zanzibar utakaomchagua rais, wawakilishi na madiwani unatarajiwa kufanyika tarehe 31 Octoba na matokeo yake yanatarajiwa kutangazwa siku hiyo hadi tarehe pili Octoba mwaka huu

TUME YA UCHAGUZI ZENJI YAONGEZA DHAMANA KWA WAGOMBEA KITI CHA URAIS KATIKA UCHAGUZI WA 2010


ZANZIBAR:

Tume ya uchaguzi Zanzibar imepandisha dhamana ya wagombea wa kiti cha urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu kutoka shilingi milioni moja hadi milioni tatu.

Akizungumza na Zenji Fm radio juu ya ratiba ya uchaguzi mkuu, afisa habari wa tume hiyo Idriss Haji Jecha amesema kiwango hicho kimeongezwa kutokana na hali ya kifedha ya watu wanaotaka kugombania urais na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.

Aidha tume hiyo pia imepandisha dhamana kwa nafasi za uwakilishi kutoka shilingi elfu 50 hadi laki tatu na nafasi za udiwani kutoka shilingi elfu 15 hadi shilingi elfu 50

Kwa mujibu wa taarifa ya tume hiyo uteuzi wa wagombea kwa nafasi zote tatu utafanyika tarehe 03 Septemba ambao utatanguliwa na uchukuwaji wa fomu utakaonza tarehe 10 hadi tarehe 30 Agosti.

Kampeni za wagombea zitaanza tarehe 10 Septemba hadi tarehe 30 Octoba ambapo vyama vitakavyoweka wagombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar vitawasilisha ratiba zao za kampeni kwa tume hiyo si zaidi ya tarehe 30 Agosti.

Aidha tume ya uchaguzi imesema upigaji kura utafanyika siku ya Jumapili ya tarehe 31 Octoba na matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa kuanzia tarehe 31 hadi tarehe 02 Octoba

Thursday, April 22, 2010

ITAKUKUTA NA WEWE


Habari yako ndungu unaetembelea Blog hii. kwa takribani wiki moja hivi tumeshindwa ku upload story au habari . Hii ilikuwa kutokana na mabadiliko ya Technology.. Hii imetukuta sisi Zanzibar . Kwa wale wote waliokuwa wakitumia window xp service pack 2 basi walikuwa hawawezi kusoma email ya yahoo . hotmail wengine hata kufungua face book au ku upload chochote kwenye mtandao. Ndio maana tulikuwa tunasumbuka sana Hadi tumelitaftia ufumbuzi suala hili. Kumbe ni Windo xp service pack 2 imepitwa na wakati na nilazima uwe na Windo xp service pack 3 au Window vister au window 7 .. Endapo na wewe imekutokea basi usishangae just upgrade yr window .

Naamini hii ni kutoka kwa Microsoft wenyewe. So na wewe itakukuta tu.

Kuanzia kesho kama kawaida habari zitakuwa update . Thx

Friday, April 16, 2010

MWAKILISHI WA JIMBO LA TUMBE CUF AMTWANGA NGUMI MUUZA SAMAKI

Mwakilishi wa jimbo la Tumbe CUF,Ali Mohd Bakar huenda akafikishwa mahakani baada ya kumtwanga ngumi mchuuzi wa samaki kisa ni kudondokewa na tone la maji ya mavumba ya samaki katika gari ya abiria waliokuwa wakisafiria

Tukio hilko lilitokea juzi majira ya saa tano asubuhi huko Wingwi wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Kadhia hiyo ya aina yake ilitokea wakati wa msafara huo ambapo mchuuzi huyo Said Kombo mkaazi wa Wete alipokuwa akisafirisha biashara yake hiyo.
Akisimulia tukio hilo Bw Kombo amesema kuwa mheshimiwa huyo alimtolea maneno ya kashfa baada ya maji hayo ya mavumba kumdondokea kwa bahati mbaya na baada ya majibizano kutokana na kitendo kile aliamua kumpiga ngumi.
“Baada ya kudondokewa na maji hayo tukasimamisha gari akaenda kujisafisha lakini hatimae baada ya kurudi ndani ya gari mie nikaenda kukaa kule kulikochafuka na mimi lakini bwana huyo hakuridhika akaanza kunitolea maneno machafu,mjinga wewe,mwanaharamu,mshenzi na akaniambia kuwa vumba lako likiniingia tena nitawaangusha samaki wako,mimi kwa vile ni binadamu niakapandwa na hasira nikamwambia huwezi baada ya kumwambia hivyo akanipiga ngumi,mimi nikamuuliza je bwana mkubwa umeridhika akaniambia ndio nishakupiga na kashtaki popote”

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Kaskazini Pemba Yahya Rashid Bugi amesema kuwa kesi hiyo ilifikishwa kituo cha polisi tarehe 12 mwezi huu.
Aidha kamanda bugi amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea ambapo Bw Soud ametakiwa kupeleka mashahidi wake ili kesi hiyo ipelekwe mahakamani.

Thursday, April 15, 2010

IDADI YA WATALII IMEPUNGUA ZANZIBAR


Idadi ya watalii wanaoitembela Zanzibar imepungua kwa kwa kiasi kikubwa kuanzia March mwaka huu, hali ambayo inatishia kupungua nafasi za ajira katika sekta ya utalii.
Akizungumza na Zenji Fm radio mwenyekiti wa Jumuiya ya wawekezaji wa utalii Zanzibar Simai Mohamed Said amesema hali hiyo ni ya kawaida inayotokea katika kipindi cha mwezi wa March hadi April kila mwaka.
Hata hivyo amesema kukatika kwa huduma ya umeme kwa kipindi cha miezi mitatu na mgogoro wa kiuchumi duniani pia imepunguza idadi ya watalii wanaotembelea Zanzibar.
Amesema katika kukabiliana na hali hiyo jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya utalii Zanzibar inaendelea kutoa taarifa kwa mashirika ya kimataifa ya waongozaji wa wageni

TUTENGENEZEWEE SEHEM MAALUM YA SOKO LETU


Umoja wa watu wenye ulemavu Zanzibar umelitaka baraza la manispaa Zanzibar kutenga sehemu katika soko la mwanakwerekwe na eneo la biashara la Saateni ili kuwawezesha watu wenye ulemavu kufanya biashara katika maeneo hayo.
Akizungumza na Zenji Fm Radio mkuu wa mipango wa umoja huo Salma Haji Saadat amesema hali iliyopo sasa katika sehemu hizo haitoi nafasi kwa watu wenye ulemavu kufanya biashara.
Amesema watu wenye ulemavu wamehamasika kufanya biashara ili kuondokana na utegemezi katika familia zao, lakini baadhi ya taasisi hazingatii mahitaji ya watu hao katika mipango yao ya kiuchumi.
Amesema kwa mujibu wa sheria namba tisa ya kulinda haki za watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kujiendeleza kiuchumi, sheria hiyo bado haijatekelezwa kikamilifu kutokana na kutokuwepo sehumu zenye kutoa huduma kwa watu maalum

TUME IMEKATAA KURUDIA UWANDIKISHAJI ZANZIBAR


Tume ya uchaguzi Zanzibar imesema haina mpango wa kurudia aundikishaji wa wananchi katika daftari la wapiga kura licha ya idadi ndogo ya watu waliosajiliwa katika baadhi ya maeneo.
Akizungumza na Zenji Fm radio mkurugenzi wa tume hiyo Salum Kassim Ali amesema bado tume hiyo haijapanga uandikishaji mwengine baada ya kumalizika uandikishaji wa awamu ya pili
Amesema licha ya kuwepo malalamiko ya watu kunyimwa haki zao katika uandikishaji huo, lakini malalamiko hayo ni machache ikilinganishwa na uchaguzi uliopita baada ya tume hiyo kuvishirikisha vyama vya siasa kuangalia shughuli za undikishaji.
Amesema uandikishaji wa awamu ya pili unatarajiwa kumalizika Mei mwaka huu na tume ya uchaguzi inaendelea na maandalizi ya upigaji kura kwa kutoa vitambulisho kwa kila aliejindikisha katika daftari la wapiga kura.
Aidha bw. Kassim amesema mipango ya uteuzi wa wagombea na elimu ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi huo imekamilika na maandalizi mingene yanakwenda vizuri.

Wednesday, April 14, 2010

WASOMALI WAENDELEZA WIMBI LA UTEKAJI NYARA MELI


MOGADISHU:
Maharamia wa Somalia wameiteka nyara meli ya Umoja wa Falme za Kiarabu ikiwa na mabaharia 26 karibu na visiwa vya Ushelisheli iliyokuwa ikija hapa Zanzibar.
Mabaharia 10 kati ya waliomo kwenye meli hiyo ni raia wa Tanzania, 11 ni raia wa India na watano ni raia wa Pakistan.
Habari zinasema kwamba maharamia hao wameipeleka meli hiyo kwenye fukwe za Somalia.
Maafisa wa safari za baharini wa India wamesema kwamba katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, maharamia wa Somalia wameteka meli 11 ambapo mabaharia 120 wa India ni miongoni mwa watu waliokuwemo kwenye meli hizo.
Takwimu za kimataifa zinaonesha kuwa idadi ya mashambulizi ya maharamia wa Somalia katika bahari ya Hindi na Ghuba ya Aden yaliongezeka sana mwaka uliopita wa 2009 ikilinganishwa na mwaka 2008.

WATOTO WENYE ULEMAVU ZANZIBAR


Watoto wengi wenye ulemavu Zanzibar wanakabiliwa na matatizo kutokana na huduma za watu wenye ulemavu kutopewa umuhimu katika mipango na bajeti za wizara za serikali.
Mkurugenzi wa mradi wa marekebisho ya watoto wenye ulemavu Tala Mswalam Said amesema vijana wenye ulemavu wanakosa visaidiza vya kufanya shughuli muhimu za kijamii kutokana na serikali kutolipa umuhimu suala hilo..
Akifungua semina juu ya mahitaji ya marekebisho ya watu wenye ulemavu mjini hapa amesema visaidizi ni nyenzo muhimu kwa vijana wenye ulemavu zitakazowasaidia katika shughuli zao za maendeleo.
Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu ambao unazitaka nchi hizo kuweka mikakati ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kushiriki katika kujiletea maendeleo.

Hivyo amesema iko haja kwa serikali kutenga bajeti maalum kwa ajili ya kuwaendeleza watu wenye ulemavu hasa katika masuala ya kuwapatia ajira.
Nae waziri wa nchi afisi ya waziri kiongozi Hamza Hassan Juma akifungua semina hiyo amewataka wakuu wa taasisi za serikali kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu wanapoandaa mipango ya taasi zao.
Amesema serikali imeandaa sera na sheria za kuwalinda watu wenye ulemavu ili kuona kundi hilo linashiriki katika sekta zote za jamii na uchumi hasa katika suala la kupatiwa ajira.
Semina hiyo ya siku mbili imeandaliwa na taasisi ya Civil Society na kuhudhuriwa na wakuu wa baadhi ya taasisi za serikali na jumuiya za kiraia.

WALIO VUNJIWA NYUMBA ZAO KWARARA WAIJIA JUU SERIKALI


Baada ya takriban mwaka mzima kupita
tokea wananchi wa eneo la Kwarara kubomolewa nyumba zao. Baadhi ya wananchi hao leo wamejitokeza katika kituo cha Zenj fm Radio na kutoa malalamiko yao.
Akizungumza na Mwangaza wa Habari Mwenyekiti wa kamati ya waliovunjiwa Bw Khamis Hassan Ali amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wanawalazimisha kuondoka katika maeneo hayo wakati maeneo hayo kesi yake bado iko mahakamani na haijatolewa uamuzi wowote
Aidha ameiomba serikali kulifuatilia kwa kina suala hilo ili wananchi wapatiwe haki zao.
Lakini katika hali ya kushangaza Bw Khamis Hassan Ali amedai kuwa kuna baadhi ya viongozi wanaowalazimisha wananchi hao kuhama ambapo amemtaja Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi) wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr Mwinyihaji Makame…bonyeza HAPA kumsikia Bw Khamis Hassan Ali...Mwenyekiti wa kamati ya waliovunjika

Nae mkaazi wa Kwarara Bw Ali Khamis Hassan ameungana na mwenyekiti wa kamati hiyo ya waliovunjiwa kwa kusema kuwa wamevunjiwa nyumba zao kwa uonevu mkubwa huku wakiishi katika mazingira ya kusikitisha.
Katika malalamiko yake Bw Ali Khamis Hassan amesema kuwa wameshangazwa na kitendo cha sheha wa shehia hiyo pamoja na viongozi wengine kutembelea eneo linalomilikiwa na wananchi hao ambapo kwa mujibu wa Bw Ali,eneo lililotembelewa linataka kujengwa skuli. Aidha ameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kulipatia ufumbuzi suala hilo kabla amani haijavunjika.…Bonyeza HAPA kumsikia Bw Ali Khamis Hassan...Mkaazi wa Kwarara

Akimalizia malalamiko yao Bw Salum Seif Salum ambae pia ni mjumbe wa kamati ya watu waliovunjiwa na mkaazi wa Kwarara ameelekeza malalamiko yake kwa baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini na kumuomba Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh Aman Abeid Karume kuwashuhulikia viongozi aliowateua katika ngazi mbali mbali kwa vile ndio wa kulaumiwa kutokana na ubinafsi wao katika majukumu aliyowakabidhi.
Bw Salum pia ameelekeza malalamiko yake kwa baadhi ya taasisi za kutetea haki za binadamu na wasomi mbali mbali waliopo nchini kwa madai kuwa wameshindwa kutetea maslahi ya wanyonge waliovunjiwa maeneo ya Kwarara…Bonyeza HAPA kumsika Salum Seif Salum...mjumbe wa kamati ya watu waliovunjiwa Kwarara

Baada ya kuwasikia wananchi hao wakilalamikia kitendo cha baadhi ya viongozi kuchukua eneo hilo,Mwangaza wa Habari ulifanya juhudi za kumtafuta Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini,ambae yeye amesema kuwa si kweli kuwa amechukua eneo hili kwa vile yeye hana uwezo wa kuchukua ardhi wala hana mamlaka hayo Bonyeza HAPA kusikia majibu ya sakata lote kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyihaji Makame

MVUA ZALETA ATHARI ZANZIBAR


Mvua za masika zimeanza kunyesha nchini na kuathiri baadhi ya maeneo mbali mbali na hatimaye wananchi wengine kukosa makaazi.
Kutokana na maafa hayo na mengine Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanzisha kitengo mahsusi cha maafa ambacho kipo chini ya Ofisi ya Waziri Kiongozi.
Tukiachana na suala la mvua maafa mengine mbali mbali yamewahi kutokea nchini na kitengo hicho kimekuwa mstari wa mbele kuwasaidia na kuwaelimisha wananchi juu ya madhumuni ya kitengo hicho.
Mwangaza wa Habari leo umeingia katika kitengo hicho na kutaka kufahamu tahtmini ambayo imefanyika kwa wale walioathirika na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa.
Katika mazungumzo yake na Mwangaza wa Habari waziri wa nchi ofisi ya waziri kiongozi Hamza Hassan Juma ambapo kitengo cha maafa kipo katika ofisi yake amesema kuwa kwa sasa kitengo cha maafa kinafanya tathmini ya walioathirika lakini tathmini kamili itatolewa baada ya mvua hizi za masika kumalizika...Bonyeza HAPA kumsikia Mhe HAMZA AKIZUNGUMZIA ATHARI ZA MVUA

Tuesday, April 13, 2010

SEMBE BOVU LAZUIWA KUINGIA ZANZIBAR


Zaidi ya robo tani ya unga wa sembe aina ya Jembe kutoka nchini Kenya umezuiliwa kusambazwa Zanzibar baada ya kubainika kuwa haufai kwa matumizi ya binadamu.
Mrajisi wa bodi ya chakula, dawa na vipodizi Zanzibar Dr. Burha Othaman Simai amesema sembe hilo limeingia nchini bila ya kusajiliwa na inasadikiwa limeshushwa katika bandari isiyo rasmi.
Aidha bodi hiyo imebaini kuuzwa kwa vipodozi vilivyopiwa marufuku na kuwataka wananchi kuwa wangalifu wanaponunua bidha hizo ili kuepukana na madhara

MAKAMBA...AJIBU SHUTUMA ZA WAPINZANI JUU YA KUKUSANYA MABILIONI


Chama cha Mapinduzi CCM tarehe 8 April mwaka huu kulizindua kampeni ya uzinduzi wa kukichagia chama hicho kwa njia ya jumbe mfupi wa simu (SMS) ambapo chama hicho kinategemea kukusanya shilingi bilioni 50.
Kufuatia hatua hiyo amabyo imetiliwa shaka na baadhi ya vyama vya siasa kikiwemo cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Daima la aprili 1 mwaka huu.
Kwa mujibu wa gazeti hilo Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, aliielezea hatua hiyo ya CCM kuwa ni kielelezo cha namna chama hicho tawala kilivyo mstari wa mbele kuvunja Sheria ya Gharama za Uchaguzi iliyosainiwa kwa mbwembwe na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni.
Ukiachana na CHADEMA, chama cha wananchi CUF nacho kimeungana na CHADEMA ambapo wamedai kuwa hatua hiyo ni uvunjifu wa sheria ya gharama za uchaguzi iliyosainiwa na Rais Kikwete. Chama cha CUF kimedai kuwa hawaamini kuwa CCM ina uwezo wa kuchagisha milioni 40 kutoka kwa wanachama wake wa kawaida na badala yake fedha hizo zitapatikana kupitia kwa wafanyabiashara ambao wanatumia fedha zao kwa maslahi yao binafsi bonyeza hapa kumsikia Bw JUMA DUNI

Kufuatia madai hayo Mwangaza wa Habari ulimtafuta Katibu Mkuu wa CCM,Bw Yussuf Makamba ambapo alipoulizwa juu ya hilo alijibu kama ifuatavyo bonyeza hapa kumsikia MAKAMBA

ZOEZI LA UANDIKISHAJI NA MIZENGWE YAKE


Awamu ya pili ya uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura unaoendelea visiwani Zanzibar umekumbwa na malalamiko ya kutokuandikishwa kwa baadhi ya wananchi wenye sifa zote zilizowekwa kisheria pamoja na kukataliwa na masheha wakidai hawawatambui au hawako katika shehia husika.
Mwangaza wa habari wa Zenj fm ilibahatika kuzungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Cuf taifa na Mwakilishi wa Kuteuliwa Juma Duni Haji ambaye ametoa malalamiko kutokana na vitendo walivyofanyiwa baadhi ya wananchi ambao walijitokeza katika uandikishaji huo na kukataliwa.
Naibu katibu mkuu huyo wa CUF anazungumzia jinsi zoezi la uandikishaji lilivyokuwa katika maeneo ya Chumbuni, Kituo cha Mabanda ya ng’ombe ambako uandikishaji wake ulifikia tamati kwa siku ya jumapili iliyopita Bonyeza Hapa kumsikia Bw JUMA DUNI

Kufuatia malalamiko hayo Mwangaza wa habari ulimtafuta afisa habari wa tume ya uchaguzi Zanzibar Maalim Idrissa Haji Jecha mabae amesema kuwa tume ya uchaguzi inafanya juhudi za kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapatiwa haki yake kwa vile tume na maafisa wake hawana mamlaka ya kumkatalia mtu bila sababu za msingi Bonyeza hapa kumsikia Bw IDRISSA HAJI JECHA

Monday, April 12, 2010

BEI YA SUKARI YAZIDI KUPANDA ZANZIBAR


Bei ya sukari bado Zanzibar imeonekana kuwa juu licha ahadi zilizotolewa na maafisa wa idara ya biashara Zanzibar kulipatia ufumbuzi tatizo hilo la kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wetu alietembelea soko kuu la mjini Chakechake Pemba kilo moja ya sukari inauzwa kati ya shilingi elfu moja na 500 hadi elfu moja na 600.
Aidha katika maduka ya reja reja ya manispaa ya mji wa Zanzibar na maeneo ya karibu kilo moja ya suakari inauzwa kati ya shilingi elfu moja na 400 hadi elfu moja na 500.
Hivi karibuni uongozi wa idara ya biashara Zanzibar umeimbia Zenji Fm radio kwamba kupanda kwa bei ya sukari kunatokana na uzalishaji mdogo wa bidhaa hiyo pamoja na kupanda bei katika soko la dunia.
Bidhaa nyingine kama vile unga wa ngano uko katika bei ya wastani ya shilingi 800 kwa kilo, lakini kilo moja ya mchele wa kawaida inauzwa kati ya shilingi 900 hadi elfu moja wakati mchele wa Mbeya unauzwa kati ya shilingi elfu moja na 300 hadi elfu moja na 500.

CUF IMESEMA ZAIDI YA WANANCHI MIA MBILI NA 82 WAMEKATALIWA KUANDIKISHWA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI KUTOKANA NA UTASHI WA KISIASA.


Chama cha wananchi CUF kimesema zaidi ya wananchi mia mbili na 82 katika majimbo ya Dimani, Magogoni na Mwanakwerekwe wamekataliwa kuandikishwa katika daftari la wapiga kura awamu ya pili kutokana na utashi wa kisiasa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF Juma Said Sanani amedai wananchi hao wanavyo vielelezo vyote vinavyowaruhusu kuandikishwa, lakini wamekosehwa haki yao hiyo ya kidemokrasia.
Akizungumza na Zenji Fm radio amesema miongoni mwao ni mia moja na 85 kutoka jimbo la Dimani, 36 jimbo la Magogoni na 43 jimbo la Mwanakwerekwe.
Aidha amedai masheha ambao ni wakala wa tume ya uchaguzi ndio waliopinga kuandikishwa kwa watu hao kwa kile alichodai kutokana na itikadi zao za kisaisa
Kazi za uandikishaji katika daftari la wapiga kura awamu ya pili hivi sasa zinaendelea katika majimbo ya Rahaleo na Kikwajuni wilaya ya mjini

VITAMBULISHO VYA UKAZI VYALETA UTATA ZANZIBAR

Afisi ya vitambulisho vya ukaazi imelalamikiwa na baadhi ya masheha kwa kuwapatia vitambulisho vya mzanzibari mkaazi wananchi bila kupatiwa fomu kutoka kwa masheha.
Malalamiko hayo yamejitokeza katika baadhi ya vituo vya uandikishaji vya majimbo ya Kwamtipura, Chumbuni na Amani baada ya badhi ya vijana kunyanganywa vitambulisho vyao na masheha kwa madai ya kuvipata kwa udanganyifu.
Sheha wa shehia ya Kwamtipura, Machano Salum Khamis amesema wananchi wanaomba vitambulisho vya ukaazi hupatiwa barua za masheha, lakini hivi sasa wanaomba moja kwa moja katika afisi ya vitambulisho.
Amesema hali hiyo imekuwa ikisababisha udanganyifu na hivyo amechukua uwamuzi wa kuwanyanganya vitambulisho hivyo baadhi ya vijana waliokwenda kujiandikisha kwa madai ya kivipata visivyo halali.

Hata hivyo vijana wengine walirudishiwa vitambulisho vyao baada ya kufika afisini kwake
Kazi za undikishaji zinaendelea katika majimbo ya Rahaleo, Mjimkongwe na Kikwajuni baada ya kumalizika jana katika majimbo ya Chumbuni, Kwamtipura na Amani.
Hata hivyo kazi hizo za uandikshaji katika majimbo hayo zimekumbwa na tatizo la wananchi kutojua mipaka ya majimbo yao na kusababishwa kukataliwa kuandikishwa katika daftari la wapiga kura.
Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi Zanzibar zaidi ya watu laki tatu na elfu 65 wameandikishwa katika daftari la kupiga kura katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni afisa wa habari wa tume hiyo Idrissa Haji Jecha amesema idadi kubwa ya watu wamejitokeza kujiandikisha katika awamu ya pili inayomalizia katika baadhi ya majimbo.

RAIS WA ZANZIBAR DR. AMANI ABEID KARUME AMETUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA RAIS WA POLAND


Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. amani Abeid Karume ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha rais Lech Kaczynski wa Poland baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kuanguka nchini Urusi ikiwa na zaidi ya abiria 90 akiwemo mkewe.
Katika salamu hizo Dr. Karume ameelezea masikitiko yake na kushtushwa na kifo hicho pamoja na maafisa wengine wa serikali ya Poland waliokuwemo kwenye ndege hiyo.
Rais Karume ametuma salamu hizo kwa kaimu rais wa nchi hiyo pamoja na raia wa Poland.
Amesema wananchi wa Zanzibar wanaungana na wenzao wa Poland katika maombelezi ya msiba huo na kusema uhusiano wa nchi mbili hizo utaendelezwa zaidi

TATIZO L A MAFUTA ZANZIBAR

Idara ya nishati na madini Zanzibar imesema ukosefu wa vifaa vya kuchunguzia ubora wa mafuta ya petroli, na Dizeli kunachangia kuingia kwa nishati hiyo chini ya kiwango kinachokubalika.
Mkurugenzi wa idara hiyo bwana Zuberi amesema hali hiyo inaleta usumbufu kwa wateja wanatumia mafuta hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar amesema baada ya kukosekana kwa vifaa hivyo kigezo kikubwa kinachotumika ni makisio yanayotokana na nyaraka za kusafirishia nishati hiyo.
Tatizo hilo limejitokeza baada ya madereva mbali mbali wanaoendesha vyombo vya moto kulalamika kuwa mafuta yanayoingia nchini hayako katika kiwango bora na kusababisha vyombo hivyo kuharibika haraka.
Mkurugenzi huyo amefahamisha kwa upande wa Tanzania bara wanayo maaabara ya aina hiyo kupitia Shirika la TBS ambapo wafanyabiashara wanaoingiza mafuta chini ya kiwango huchukuliwa hatua za kisheria.
Hivyo amesema Zanzibar inahitaji kuwa na vifaa hivyo ili kuwalinda watumiaji wa nishati hizo.

WAZIRI KIONGOZI AMESEMA MATATIZO YA MUNGANO KATIKA SEKTA ZA FEDHA NA BIASHARA YANAHITAJI MFUMO MAALUM


Waziri kiongozi wa serikali ya Mapinduzi Zaznibar Shamsi Vuai Nahodha amesema matatizo ya mungano katika sekta za fedha na biashara yanahitaji mfumo maalum wa utatuzi wake ili kuleta maslahi kwa pande mbili za muungano
Amesema licha tume ya pamoja ya fedha ya Muungano kuwasilisha ripoti yake kwa serikali zote mbili ya mgawanyo wa mapato, lakini hatua hiyo itasaidia kutatua tatizo hilo kwa asilimia 60.
Waziri kiongozi Nahodha amesema katika mahojiano maalum na redio Uhuru huko afisini kwake.
Kuhusu hali ya baadae ya Zanzibar itavyofaidika na Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema bado itakabiliwa na changamoto za kitaalamu na mitaji ambazo zinaweza kukwamisha biashara za Wazanzibari.
Hata hivyo, amesema Zanzibar inaweza kufaidika kama itakuwa na viwanda vidogo vidogo vya samaki na maabara za kuchunguza bidhaa hizo zitazosafirishwa nje ya Jumuiya hiyo.

Sunday, April 11, 2010

UWANDIKISHAJI PEMBA WAENDELEA VIZUZI


Kazi za uwandikishaji awamu ya pili katika daftari la kudumu la wapiga kura kisiwani Pemba zimeelezewa kwenda vizuri huku kukiwa na idadi kubwa ya watu wanaojiandikisha.
Afisa Uandikishaji Wilaya ya Chake Chake Rashid Suleiman Omar amesema wafanyakazi wa tume ya uchaguzi wamekuwa wakipata ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi wa maeneo ya uandikishaji.
Amesema wananchi wote wenye sifa wanaandikishwa na hakuna mtu ambae anasifa na aliekosa haki yake ya kujiandikisha kama mpiga kura na kuwataka wananchi wenye sifa kujitokeza katika uandikishaji huo unaoendelea katika wilaya ya Chakechake.
Katika jimbo la Chakechake jumla ya wananchi elfu nne, 438 wa Shehia tisa za jimbo hilo wamejiandikisha wakiwemo wanawake elfu mbili, 388.

Friday, April 9, 2010

MWALIMU ‘FATAKI’ AVURUGA MABINTI SKULI YA VIKOKOTONI .AMKATISHA MASOMO BINTI KIDATO CHA TATU

SASA imedhihirika kwamba Mwalimu wa Sekondari ya Vikokotoni mjini hapa, ni kitangi au fataki baaada ya kuooa mwanafunzi wa kidato cha tatu wa skuli huyo, mwenye umri wa miaka 16.

Habari za uhakika kutoka vyanzo mbalimbali, vinasema kwamba mwanafunzi huyo aliyegeuzwa mke, anaitwa Safia na mwalimu huyo, Fadhili Mkali, amejitetea kuwa aliona binti wa nyumbani.

Mzazi wa mtoto huyo, alilithibitishia NIPE HABARI, kwamba: “Nimeozesha binti yangu,” baada ya msichana huyo kwenda kumshataki kwa kadhi juu ya suala hilo .

Mzazi huyo ambaye kwa sasa aliomba kutotambulishwa gazetini, alisema: “Nimeamua kuozesha baada ya kushindwa kwa watu wote kumshawishi binti kuacha kuolewa. Ilishindikana kabisa.”

“Wajomba zake na shangazi zake na watu wote wamekataliwa na tukaamua kumuozesha, lakini bado yuko nyumbani kwa kisingizio cha kumaliza mambo yao . Bado hajamchukua,” alisema baba huyo aliyeozesha juzi Jumatano.

“Niliona bughuza kunifikisha kwa kadhi kunishitaki,” alisema mzee huyo aliyekuwa na hali ya mashaka na wasiwasi wakati angongea na mwandishi wetu.

Akizungumza na Zenjfm , kama atakubali msaada sheria ili mtoto huyo andelee na masomo, alisema hana haki ya kumrithi kwa walivyokubaliana na mtoto wake huyo baada ya kumfungisha ndoa.

Akisimulia kuhusu suala hilo , mama mzazi wa mwanafunzi huyo, alisema: “Baada ya hali kuwa mbaya, Safia alikuwa hasemi na mtu humu ndani.”

Alisema kuwa mwalimu huyo alikuja yeye na kusema kuwa anataka kuolewa na huyo kijana ambaye inaelezwa kuwa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na baadhi ya wanafunzi.

Mama huyo ametoa wito kwa wazazi wengine kuwa makini na mabinti zao kwake wa kwake, ilishindikana baada ya kutaka kuolewa na mwalimu huyo.

Mjomba wa mtoto huyo, ambaye pia aliombwa asitambulishwe kwa jina gazetini, alisema: “Sisi tunamwambia tunahitaji msaada kwani mwalimu huyu ana kesi tatu kwa watoto tofauti kwani sisi wizara ya elimu ilishindwa kutusadia badaa ya sisi kwenda wizara ya bila ya msaada wowote mpaka sasa.”

Mwenyekiti wa kamati ya skuli ya Vikokotoni, alithibitisha kuolewa kwa binti huyo akisema: “Suala hili tumelipokea na sasa tunakutana ili kulifanyia uamuzi wa jambo hilo ,” alisema na kukata simu.

Bi. Mwamidi kutoka Wizara ya Elimu, alisema wamepokea kesi hiyo kwa ajili ya kushughulikia katika misingi ya ushauri na malezi.

Alithibitisha kuwa mwalimu huyo walimwita na kufanya mahojiano na akajibu alimkuta nje ya geti la shule na kumwambia juu ya kutaka kumuoa na kwamba hakudhani kama mwanafunzi.

Wizara ya elimu ilipendekza kuwa mwalimu apewe onyo na kupewa uhamisho.

Wakati huo wizara ya elimu imethibitisha kuwa wakati inashulikia jambo hilo tayari kuna kesi mbili hazijashughulikiwa zinazomuhusu mwalimu huyo juu ya uhusiano wa kimepanzi na mwalimu.

MTOTO WA RAIS KARUME AZUA BALAA LA SHAMBA NUNGWI

AHMED, mtoto wa Rais wa Zanzibar , Amani Abeid Karume, ametumbukia kwenye kashfa ya kunyang’anya ardhi baada ya kupora shamba kubwa Kaskazini Unguja, NIPE HABARI, limearifiwa.

Mtoa habari wa eneo hilo , alisema kwamba malalamiko yao serikalini kupitia Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himid, akidai ya kuwa “Ahmed Amani Abeid Karume amevamia shamba lao.”

Mlalamikaji huyo alitoa madai hayo kupitia kituo cha Redio cha Zenj FM, akisema: “Sisi ni wamiliki wa shamba la huko, lakini limevamiwa na mtu anayeitwa Ahmed Amani Abeid Karume,” lakini watendaji husika serikalini hawaonyeshi kushtushwa.

Mdai huyo, Bi Fatma Ali kutoka familia ya Mzee Diku ya Nungwi, alisema ameshutushwa na kuvamiwa kwa shamba usiku wa manane na mafundi waliojitambulisha kuwa “Wametumwa na Ahmed Amani Abeid Karume.”

“Sisi tuna nyaraka za muda mrefu kumiliki eneo hilo ambalo hatulitumii,” alisema na kuonyesha nyaraka hizo zenye namba ya usajili 1783 uliotolewa 22 Desemba, 1935.

“Tukienda kwa wahusika tunambiwa kuwa amechukua mtoto wa mkubwa,” alisema Bi. Fatma na kuongeza: “Mtoto huyu amepeleka mafundi usiku wa manane ili kuanza kazi ya kujenga.”

Alisema: “Tayari ameshapeleka suala hilo kwa viongozi wote akiwemo waziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Kuwaambia kuwa mtoto wa rais amepora ardhi ya raia wanyonge.”

Akielezea hatua alizozichukua ni pamoja na kuwauliza viongozi wote akiwemo Sheha wa Nungwi pamoja na kupeleka barua hata kwa Waziri Kiongozi, Shamvi Vuai Nahodha, lakini hata hivyo taarifa zinasema kwamba waraka wao haukufika.

Alisema japo aliandika barua kwa waziri ilichukua muda mrefu bila ya kupata majibu na zaidi anaona mafundi wamepelekwa kuanza ujenzi unaoonekana utakuwa wa gharama kubwa.

Sheha wa eneo hilo, aliwambia: “Mtoto wa rais ndiye alikuja na maofisa wa Ikulu pamoja na mkuu wa kutuo cha polisi Nungwi na kutuambia kuwa alipewa shamba hilo kwa barua ya mkurugenzi wa ardhi.”

Hata hivyo, Mzee Diku, alisema: “Hakuna chochote tulicholipwa.”

Fundi Mkuu wa ujenzi huo, Abdallah Mkanda alithibitisha: “Ndio, kweli tumetumwa na mtoto huyo wa rais.”

Alikubali kusitisha ujenzi mpaka “tajiri wao”, Ahmed Aman Abeid Karume, atakapokwenda kumaliza matatizo hayo huku akisema: “Sisi tumepewa kila aiana ya msaada tunaotaka ili waweze kuanza kazi, lakini tulikuja hapa usiku kwa sababu tulichelewa kupeleka vifaa katika eneo hilo .”

Sheha wa shehia hiyo ya Nungwi amefafanua, alikubali kuwa “mashamba hayo ni mali halali kwa watu wa Nungwi kwani yanalengwa kugaiwa kwa wazaliwa wa eneo hilo tu.”

Akifananua kuwa eneo hilo , lilikuwa limetolewa kwa Kaligendo kabla ya kupewa Nungwi Peninsula ambao wote walishindwa kuliendeleza ndipo akapewa Ahmed.

Lakini akasema: “Utaratibu huu sasa mimi nimeukuta na masheha wenzangu wameniambia kuwa watu wameshalipwa, lakini naogopa kulalamika kwa kuwa mtoto wa rais,” alisema sheha huku akionyesha kuishiwa nguvu juu ya suala hilo .

“Mimi najua kuwa kweli shamba hili amepewa Ahmed, lakini mimi nalaumu watu wa wizara ya ardhi kwa kuwagawa eneo hilo bila ya kuwatarifu wale wanaolishughulikia eneo hilo .”

Akaifafanua juu ya kadhi hiyo sheha huyo amesema: “Kwa kweli, kutokana na mkono wa rais kuwako hapa, sina la kusema hata kidogo. Kashapewa mtoto wa rais, mimi sina mkono wangu,” alisema sheha aliyeteuliwa mwaka 2008 katika shehia hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Bw. Pemba Juma Khamis, alisema hajapokea malalamiko bali amesikia tu kwa watu, lakini alifafanua kuwa eneo hilo amepewa mtu nyeti kabisa lakini ukweli suala hili tukukutane mimi na wewe nitakwambia juu ya ukweli wa suala hilo .”

Akizungumza kwa pozi na taratibu, Waziri Himid, alisema kwa ukali wa maneno: “Kweli nimelipokea suala hili, lakini anahitaji muda kulishuhulikia suala hili kwa umakini zaidi.”

Juhudi za kumpata moja kwa moja Ahmed, zilishindikana lakini kama yake, Abeid aliyeombwa kumsaka pengine atoe majibu, akasema: “Sijampata kwenye simu hivyo tutafanya jitahada zaidi kumtafuta juu ta suala hilo .”

Safu hili lilimsaka tena Abeid Karume, saa chache kabla ya kuingia mtamboni, kwa mara pili, alijibu: “Bado sijampata.”

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA RAIS JAKAYA KIKWETE AMESEMA

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi taifa rais Jakaya Kikwete amesema njia zilizobuniwa na chama hicho za kukusanya fedha za kugharamia uchaguzi kwa wagombea wake hazitakiuka sheria ya gharama za uchaguzi aliyoitia saini hivi karibuni.
Amesema fedha hizo zitakazochangwa na wana CCM matumizi yake yatakuwa wazi kwa kila mgombea wakati wa kampeni ili kuona sheria ya gharama za uchaguzi haikiukwi.
Akizungumza katika uzinduzi wa mfuko wa gharama za uchaguzi kwa CCM mjini Dar es Salaam rais Kikwete amewataka wanachama, wafuasi na wapenzi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kuchangia mfuko huo kupitia simu za mkononi…
Aidha mwenyekiti huyo amesema fedha hizo shilingi bilioni 40 sio kwa ajili ya uchaguzi wa urais pekee bali pia zitatumika kwa wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani kupitia chama hicho.Mwenyekiti huyo pia amewataka wana CCM waliojiandikisha kupiga kura kujiorodhesha katika daftari la chama hicho ili kujua idadi ya wapiga kura wake.
Chama cha Mapinduzi CCM kinatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 40 kuendeshea kampeni zake za uchaguzi kwa wagombea wa urais, uwakilishi, ububnge na udiwani kwa nchi nzima.
Katika kampeni hizo chama cha CCM kinatarajia kunua gari 26 na kuzigawa kwa kila mkoa zitakazosaidia kuendeshea kampeni kwa wagombea wake.
Hotuba ya uzinduzi huo wa uchangiaji uliofanywa na rais Kikwete usiku huu imetangazwa moja kwa moja kupitia hapa Zenji fm.

MAHAKAMA YA RUFAA TANZANIA IMEKAMILISHA UWASILISHAJI WA HOJA ZA PANDE MBILI DHIDI YA RUFAA YA SERIKALI YA KUPINGA UWAMUZI WA MAHAKAMA KUU

Mahakama ya rufaa Tanzania imekamilisha uwasilishaji wa hoja za pande mbili dhidi ya rufaa ya serikali ya kupinga uwamuzi wa mahakama kuu kutowa uwamuzi wa kuruhusu mgombea binafsi katika uchaguzi.
Kesi hiyo ilifunguliwa na mwenyekiti wa chama cha Democratic Party Mchungaji Chstopher Mtikila ambae amesema uwamuzi wa rufaa hiyo utakuwa wa kihistoria katika mustakabali wa siasa za Tanzania.
Baada ya kusikiliza maoni ya marafiki wa mahakama ya rufaa jopo la majaji wa mahakama hiyio lililoongozwa na Jaji mkuu wa Tanzania Agostino Ramadhan limefunga rasmi kupokea hoja za pande zote mbili kati ya mkata rufani na mjibu rufani.
Umuzi wa rufani hiyo unatarajiwa kutolewa katika siku itakayotangazwa na mahakama hiyo ya rufani.
Akizungumza na VOA Mchungaji Mtikila amesema iwapo hukumu ya mgombea binafsi itasimama Tanzania itaanza kuona mwanga mpya wa kupanuka demokrasia zaidi na kuondoa ukiritimba wa vyama katika uchaguzi……Awali marafiki wa mahakama ya rufaa waliotoa maoni yao wamepinga mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kama ilikuwa sahihi kutoa hukumu ya kushiriki kwa mgombea binafsi katika uchaguzi.

NI MUHIM WADAU

Habari yako ndugu unaetembelea Blog gii.. Blog hii leo ni siku ya pili tokae kwenda hewani. Jana ndio nimeanza kuitengeneza . Nataka mchango wako wa mawazo nini na nini unataka kukisoma kwenye blog hii. Sisi tuna Radio ambayo ndio ipo Zanzibar Inaitwa Zenjfm 96.8 fm. Pia tuna gazeti la Nipe Habari. Kwa maana hiyo Tuna habari nyingi sana . Kijamii kisiasa michezo. burudani habari za ndanii na mambo mengi sana . Sasa sisi tanataka kujua kutoka kwako Unataka kusoma nini na kuona nini kwenye blog hii . Habari gani zaid zichukue nafasi . Naomba tumasiliane kwa djside_dj@yahoo.com Au andika kwenye comment sehemu hii. Ahsante mdau. Tegemea kupata habari zenye uhakika

KARUME KUELEKEA UNGEREZA LEO


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume leo anatarajiwa kuondoka nchini na kuelekea Uingereza kwa ziara ya serikali.
Katika ziara hiyo, Dr. Karume anafuatana na mkewe Mama Shadya Karume pamoja na maafisa wengine wa serikali.
Taarifa kutoka ikulu ya rais haikutaja muda wa ziara hiyo, lakini imesema Dr. Karume ataagwa leo na viongozi wa serikali katika uwanja wa ndege wa Zanzibar kuelekea nchini Uingereza.

RAIS JAKAYA KIKWETE AMEWAONYA BAADHI YA VIONGOZI WA CHAMA HICHO KWA KUANZA KAMPENI ZISIZO RASMI KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU UJAO.


Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM rais Jakaya Kikwete amewaonya baadhi ya viongozi wa chama hicho kwa kuanza kampeni zisizo rasmi kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.
Rais Kikwete amesema kampeni hizo zinavunja kanuni na katiba ya CCM ambayo inahimiza ustawi wa demokrasia ndani ya chama na nchi.
Rais Kikwete amesema hayo katika ufunguzi wa semina kwa viongozi wandamizi wa chama hicho mjini Dar es Salaam katika ukumbi wa Karimjee.
Mwenyekiti huyo amesema vitendo vya aina hiyo vinaweza kuleta mgawanyiko miongoni mwa wafuasi wa chama hicho na ndani ya chama chenyewe.
Katika kutekeleza mkakati mpya ndani ya CCM, chama hicho kitatumia utaratibu mpya wa kuwapata wagombea wa uchaguzi mkuu badala ya utaratibu wa zamani.

Thursday, April 8, 2010

UMEME ZANZIBAR BADO TATIZO


Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema hali ya umeme katika kisiwa cha Unguja bado sio nzuri licha ya matengenezo makubwa yaliofanywa hivi karibuni baada ya huduma hiyo kukatika kwa kipindi cha miezi mitatau.
Waziri wa maji ujenzi, nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid amesema ili kuepukana na hali hiyo amewataka wananchi kupunguza matumizi ya umeme yasio kuwa ya lazima.
Amesema serikali inaendelea na juhudi za kupata uemem wa hakiba ili kukabiliana na tatizo hilo na kusema kazi za ujenzi wa kuweka majenerata ya kuzalisha umeme wa dharura zinaendelea katika eneo la Mtoni.
Amesema majenerata hayo yanayotarajiwa kuwasili nchini hivi karibuni yatakidhi mahitaji ya umeme kwa asilimia 50 Akizungumzia mradi wa kuweka waya mpya wa umeme unaofadhiliwa na serikali ya Marekani waziri Mansour amesema mkandarasi wa ujenzi huo ameshapatikana na utiaji wa saini unatarajiwa kufanyika mwezi uajao kwa ajili ya utengenezaji wa waya huo na kulazwa.
Hata hivyo waziri Mansour amewataka wananchi kutojenga katika eneo linalopita mdaradi huo ili ujenzi wa mradi huo usichelewe

MARUFUKU SHOW ZA MAGARI ZANZIBAR


Jeshi la polisi katika mkoa wa kaskazini Unguja limepiga marufuku show za magari zinayofanyika Pwani Mchangani kwa madai ya kutokuwepo taarifa zozote za mashindano hayo.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo Mselem Masoud Mtulia amesema taratibu za sheria za mchezo huo bado hazikufuatwa na kuwataka wandazi wa maonesho hayo wafuate sheria.
Akizungumza na Zenji Fm radio kamanda Mtulia mesema jeshi la polisi katika mkoa huo liko tayari kutoa ulinzi endapo wandalizi wa mashindano hayo watafuata sheria na tarabu za mchezo huo